Watumiaji wa mitandao wanaopotosha mazuri ya Serikali wapigwa na kitu kizito

 

Wakati taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu,Tarehe 29 Oktoba 2025  kuna baadhi ya watu wanaotumia maarifa yao vibaya hususan kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwahadaa Watanzania wasione mazuri na kutoka ridhaa ya uchaguzi wa amani na huru.

Kundi hili linajaribu kuchafua hali ya hewa kwa kudai kuwa hakuna kilichofanywa na Serikali, huku likipuuza ukweli wa miradi na mafanikio yanayoonekana kwa macho.

Mwaka 2021, baada ya kupoteza Rais wa Awamu ya Tano, Watanzania wengi walijiuliza kwa hofu juu ya uwezo wa uongozi mpya. Leo, miaka minne baadaye, majibu yako wazi: Hakuna mradi uliokwama. Elimu bure inaendelea, SGR inakimbia, Bwawa la Nyerere (JNHPP) limekamilika na TASAF bado inagusa maisha ya mamilioni.

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amethibitisha kwa vitendo kuwa uongozi ni zaidi ya maneno; ni ujasiri, weledi, na maono. Ameweka msingi wa uchumi jumuishi unaomgusa kila Mtanzania, huku akidumisha umoja wa kitaifa na misingi ya Muungano wetu wa kihistoria.

Wale wanaotumia mitandao kudai kuwa wanatetea Watanzania, wanapaswa kuangalia rekodi safi ya Serikali ya Awamu ya Sita, ambayo imetekeleza Ilani ya CCM ya 2020–2025 kwa vitendo na kufikia mafanikio makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Matawi ya Mafanikio Kila Sekta

Mafanikio ya kiuchumi na kijamii yaliyopatikana licha ya changamoto za UVIKO-19 ni dhibitisho la uongozi thabiti:Ukuaji wa uchumi umeongezeka kutoka asilimia 4.8 mwaka 2020 hadi 5.4 mwaka 2024.Miradi ya uwekezaji imeongezeka kutoka 207 mwaka 2020 (yenye thamani ya USD milioni 1,092.7) hadi 901 mwaka 2024 (yenye thamani ya USD milioni 9,313), ikizalisha ajira zaidi ya 212,000.

Katika sekta ya kilimo, uzalishaji wa chakula umeongezeka kutoka tani milioni 18.6 (2020) hadi tani milioni 22.8 (2024), na hivyo kufanya utoshelevu wa chakula kufikia asilimia 128.Kilimo cha umwagiliaji kimeongezeka kwa asilimia 82, kutoka hekta 561,383 hadi 983,466, huku matumizi ya mbolea yakiongezeka kwa asilimia 107—ikionyesha dira ya kilimo cha kisasa chenye tija.

Kwa hiyo, tarehe 29 Oktoba si siku ya kawaida, ni siku ya kuthibitisha kuwa Tanzania inaendelea kujengwa kwa amani, utulivu na maendeleo yanayoonekana. Watanzania, tutoke kwa wingi kupiga kura. Tuiandike historia kwa kalamu ya shukrani.

Chapisha Maoni

0 Maoni