Ukivinjari katika mtandao utabaini jinsi baadhi ya Watanzania wachache wanavyoitumia mitandao ya kijamii kama uwanja wa biashara ya taharuki, wakijipatia mapato kutokana na maumivu na udhalilishaji wa wenzao.
Kundi hili, lenye tabia ya Masadisti (watu wanaofurahia kuumizwa kwa wengine), limegeuza uadui na uchochezi kuwa mfumo wa mapato unaowategemea Watanzania wengi. Hapa ndipo msingi wa tatizo letu ulipo: Mtu anapata fedha kwa sababu wewe unalipa ili usome udhalilishaji huo.
Kichocheo cha
Taharuki Kina Namba ya Akaunti
Ukweli usiopingika ni kwamba, kwa wanasadisti hawa, uchochezi na taharuki vina namba ya akaunti. Wanajua kuwa maudhui ya maumivu, hasira, na udhalilishaji huwavutia wafuasi wengi na kuwafanya kulipa ili waendelee kusoma.
Lengo la kuhama kutoka kudhalilisha wasanii hadi kuchochea vurugu za kisiasa siyo kuleta mabadiliko ya kitaifa, bali ni kusambaza mtaji wao wa kifedha. Wanamwaga sumu ya chuki na migawanyiko ili wapate shilingi 1,500 kutoka kwa kila kijana, huku wakijua kuwa vurugu haijawahi kumletea yeyote faraja.
Swali tunalopaswa kujiuliza kama taifa ni hili: Je, tutaendelea kuwanunua walaghai hawa kwa kuwaingizia mabilioni ya shilingi ili tuweze kusoma hadithi za maumivu na uchochezi wanazotengeneza?Pamoja na kukiuka misingi ya kidini, kanuni za maish alakini pia kunakukiukwa kwa sheria ya ulinzi wa masuala ya faragha.
Tanzania ya Maadili:
Kukataa Mtego wa Vurugu
Wito wa busara wa Mzee Joseph Butiku, ambaye anawakilisha hekima ya kizazi cha Mwalimu Nyerere, unasisitiza kwamba amani ya Tanzania siyo bahati nasibu, bali ni mfumo uliolindwa kwa gharama kubwa. Tabia ya masadisti inayofurahia taharuki ni kinyume kabisa cha msingi wa utulivu wetu, ambao unajengwa kwa maadili, upendo, na mshikamano.
“Ni muhimu kudumisha maadili, upendo na misingi ya amani iliyojengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.”
Hii ni sauti ya tahadhari kwa wote wanaochezea msingi wa utulivu wa taifa.Mzee Butiku amewataka Watanzania wote kuepuka kushabikia maneno ya uchochezi, kauli za kugawa taifa, na propaganda za mitandaoni zinazolenga kuvuruga umoja wa nchi.
Hivyo kitendo cha kijana kulipa ili kusoma maudhui ya kudhalilisha ni sawa na kujikata mguu mwenyewe ili aombe msaada; anawapa nguvu ya kuendelea kumpa maumivu. Vurugu na uchochezi vinataka kuharibu sifa ya taifa letu la kwenda salama na kurejea salama.
Funga Bomba la Mapato
Ili kukomesha biashara hii haramu, suluhisho liko wazi na mikononi mwa walio wengi: Acha kulipa, acha kuwa mteja. Kila unapofanya 'unsubscribe' (kukata usajili), unaziba bomba la mapato la Sadist huyo na kumlazimisha kufunga biashara ya maumivu.
Hadi Lini Watanzania Wataendelea Kuwa Wateja wa Maudhui Yanayoleta Maumivu na Taharuki Katika Jamii? Ni wakati wa kuamka, kufunga pochi, na kusambaza maudhui ya amani na maendeleo, tukitumia vyema demokrasia na vikao husika katika kuwasilisha hoja na pia fungamano na vyombo vya usalama ili wakosaji waadhibiwe.
0 Maoni