Wananchi wa kata ya
Kakesio iliyoko Tarafa ya Ngorongoro Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha
watanufaika na mradi wa Maji kwa ajili ya Mifugo na matumizi ya binadamu kufuatia
Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuchimba Kisima cha
Maji chenye urefu wa mita 110 ambacho kinatarajiwa kuzalisha maji lita 80,000
kwa siku.
Uchimbaji wa Kisima hicho
ni muendelezo wa kazi nzuri inayofanya na Serikali kwa Wananchi wanaoishi
katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambapo Kisima kama hicho kimechimbwa eneo
la Mlima matiti kwa ajili ya wananchi wa Kata ya Endulen na Alaetoli na baadae
mradi kama huo utatekelezwa katika Kata ya Olbalbal ili kusaidia wananchi
kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji kwa mifugo katika
msimu wote wa mwaka.



0 Maoni