Aliyekuwa
Mbunge wa Kilwa Kusini, Selaman Bungara, almaarufu "Bwege," ameibua
mjadala mkali baada ya kutoa wito kwa Watanzania kujiepusha na maandamano
yaliyopangwa kufanyika Oktoba 29. Bungara ametahadharisha kuwa kushiriki katika
hatua hiyo kutahatarisha amani ya nchi na huenda ikawa mwisho wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katika
kauli yake, Bungara amewajibisha wananchi kutojihusisha na ghasia kwa kuwa
amani ni kitu muhimu, huku akionyesha wasiwasi kuwa "hatujui chama gani
kinaongoza, hatujui mtu anayeongoza" maandamano hayo.
Aidha,
amesema Oktoba 29 ni siku muhimu kwa taifa na wananchi wasikubali kuvuruga
uchaguzi kwa sababu binafsi za watu wasiotakia mema nchi.
Kauli hii
imepokelewa kwa hisia tofauti, hasa katika mitandao ya kijamii, huku baadhi ya
wachangiaji wakimpongeza Bwege kwa "kuona mbele," wengine wakimkosoa
vikali na kuhusisha msimamo wake na kubadili mwelekeo kisiasa.
Licha ya
ukosoaji huo, jumbe za Bwege zimepata uungwaji mkono wanaoamini msimamo wake
unalenga kulinda amani ya nchi.

0 Maoni