WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa
Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha ustahimilivu wa
Taifa dhidi ya majanga, kupitia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati na miradi
mbalimbali
Amesema
kuwa hatua hiyo itasaidia kuendelea katika kujenga ustahimilivu wa jamii dhidi
ya maafa, tutaokoa maisha, mali, na rasilimali za taifa letu.
Amesema
hayo leo Jumatatu (Oktoba 13, 2025) wakati alipotoa tamko katika maadhimisho ya
siku ya Kimataifa ya Kupunguza madhara ya maafa, katika ukumbi wa mikutano wa
City Park Garden jijini Mbeya.
Akitaja
baadhi ya hatua zilizochukuliwa, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali
imeandaa na kuhuisha nyaraka za kitaifa kuhusu maafa ikiwemo Sera ya Taifa ya
Usimamizi wa Maafa (toleo la 2025), Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa
(2022–2027) na Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa (2022).
Aidha,
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa hatua nyingine ni Kuimarisha usahihi wa
utabiri wa hali ya hewa kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), ambao sasa
umefikia asilimia 85, hivyo kusaidia kupunguza madhara ya maafa kwa zaidi ya
asilimia 30.
“Pia
Serikali time inatosha mifumo ya tahadhari ya mapema kwa kuwezesha vifaa na
teknolojia za kisasa, ikiwemo kuanzishwa kwa Kituo cha Ufuatiliaji wa Majanga
na Utoaji wa Taarifa za Tahadhari kilichounganishwa na vituo vya kikanda barani
Afrika”.
Mheshimiwa
Majaliwa ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa yenye
kuzingatia ustahimilivu wa tabianchi ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Kidunda wenye
thamani ya shilingi bilioni 329.47, Bwawa la Farkwa wenye thamani ya shilingi bilioni 312.08
pamoja na Mradi wa Maji Ziwa Victoria-Simiyu wenye thamani ya bilioni 440.
Katika
Sekta ya Kilimo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendeleza mbinu za
ustahimilivu kwa kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, mbegu bora, mifumo ya
tahadhari mapema, na ushirikiano na wakulima wadogo.
“Aidha,
Serikali imeendelea kulijengea uwezo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuwezesha
vifaa, teknolojia, na mafunzo ya kisasa ili kuboresha huduma za uokozi na
uzimaji moto”
Pia
Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika
uwekezaji unaozingatia ustahimilivu dhidi ya majanga, ikiwemo uwekaji wa bima
na utekelezaji wa miongozo ya Serikali.
Kwa
Upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
William Lukuvi amesema kuwa maadhimisho haya yana lengo la kuhamasisha ushiriki
wa wadau wote katika shughuli zausimamizi wa maafa.
Amesema
kuwa Serikali imeendelea kuratibu utoaji mafunzo kwa wataalamu wa sekta, mikoa
na jamii wakiwemovijana kuhusu usimamizi wa maafa hususanikatika hatua za
kuzuia na kujiandaa kukabilimaafa yanapotokea pamoja na kurejesha hali.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Muwakilishi wa Umoja wa Mataifa Sandra Hakim amesema kuwa
wadau mbalimbali ikiwemo Watendaji wa Serikali za Mitaa, Viongozi wa kijamii,
Asasi za Kiraia pamoja, Umoja wa Mataifa
na mashirika ya Kimataifa wamekuwa wakifanya kazi bila kuchoka kwa ajili
ya kujiandaa, kukabiliana na kurejesha hali kwenye majanga.
Awali
Mheshimiwa Majaliwa alikagua maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru
Pamoja na kumbukizi ya baba wa Taifa itakayofanyika katika uwanja wa CCM
Sokoine jijini Mbeya.



0 Maoni