Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia
Suluhu Hassan akiomba dua kwenye Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara tarehe
10 Oktoba, 2025.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia
Suluhu Hassan akiwasha mshumaa katika Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara tarehe
10 Oktoba, 2025.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia
Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika Kaburi la Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani
Mara tarehe 10 Oktoba, 2025.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan leo tarehe 10 Oktoba, 2025 ametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika eneo la Mwitongo, Wilaya ya Butiama.
Akiwa katika eneo hilo, Mhe. Dkt. Rais Samia amezuru
kaburi la Mwalimu Nyerere na amezungumza na wanafamilia wakiongozwa na Mlezi wa
familia ya Mwalimu Nyerere Chifu Japhet Wanzagi.
Mhe. Rais ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya
Chama cha Mapinduzi yupo katika Mkoa wa Mara kuanzia jana tarehe 09 Oktoba,
2025 akiendelea na kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Baada ya hapo Mhe. Dkt. Samia ameendelea na kampeni
zake leo katika Wilaya za Butiama na Serengeti katika Mkoa wa Mara na Bariadi
katika Mkoa wa Simiyu.

0 Maoni