WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 16, 2025 ni mgeni rasmi katika kilele cha
maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Tanga,
kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara.
Madhimisho
hayo ambayo hufanyika kila mwaka yanalenga kuamsha ari ya uzalishaji wa mazao
ya chakula ikiwemo yaliyoongezewa virutubishi; kuhimiza ulaji bora na kuongeza
tija ya uzalishaji wa chakula ili kujihakikishia usalama wa chakula na lishe
kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.
Maadhimisho
hayo yanakaulimbiu isemayo “Tuungane Pamoja Kupata Chakula Bora Kwa Maisha
Bora Ya Baadaye.”




0 Maoni