Katika
kuadhimisha kumbukizi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania- TAWA jana Oktoba 14, 2025, imepokea zaidi ya watalii 100 kutoka
Jumuiya ya Mtakatifu Columba kutoka Parokia ya Bikira Maria Imakulata -Msakuzi
waliokuja kujionea uzuri wa pekee wa Hifadhi ya Wanyamapori ya Pande, jijini
Dar es Salaam.
Hifadhi
ya Pande ni hazina iliyojificha, lakini leo, imefunua uzuri wake halisi.
Watalii walipata nafasi ya kipekee kujionea wanyamapori mbalimbali kama vile
Simba, Duma, Mamba, na Chatu, Pundamilia, Swala, Mbuni na Nyumbu.
Mandhari
tulivu ya misitu, sauti za ndege wa porini, na wanyama waliopo kwa wingi
ziliwafanya wageni wafurahie kila dakika ya ziara yao.
“Hatukutegemea
kuona wanyama wengi kiasi hiki tukiwa bado Dar es Salaam”, alisema Evodius
Gasper, miongoni mwa watalii kutoka Jumuiya ya Mt. Columba.
Watalii
hawa waliahidi kuwa mabalozi wa Hifadhi ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Pande.



0 Maoni