Siku ya
maamuzi Oktoba 29, 2025 inakaribia ! Kura yako ni zaidi ya kupiga mstari; ndio
njia kuu ya kuwasha injini ya maendeleo ya nchi. Tanzania inasonga mbele kwa
kuwekeza kwenye rasilimali zetu asili – bahari, maziwa, mito, na mabwawa. Hizi
si ahadi tu, ni Uchumi wa Kisasa unaokuja na ajira, biashara, na fursa nyingi
kwetu sote.
Kwa chama
tawala Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho mambo yake mengi yanakwenda yamenyooka
katika Ilani ya Chama hicho cya 2025–2030 inakuja na mipango kabambe kwa
vijana. Wamedhamiria kuongeza kasi ya maendeleo katika Uchumi wa Buluu. Hii
inathibitishwa na miradi mikubwa inayotarajiwa kama vile ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Bagamoyo na
ukamilishaji wa Bandari ya Uvuvi Kilwa.
Hizi
zitatumika kama vituo vya kuchakata na kuongeza thamani ya mazao, huku samaki
wa bahari kuu wakipakiwa, kuchakatwa, na kuuzwa kimataifa. Hapa ndipo ajira
mpya na utajiri kwa taifa zinapozalishwa.
Kura Ndio
Kiunganishi Kati ya Ahadi na Utekelezaji
Kama
ilivyokuwa enzi za Kura Tatu ambapo kura iliamua mwelekeo wa kisiasa, leo kura
ndio inahakikisha miradi hii inatoka kwenye karatasi na kufika mtaani kwako.
Ikumbukwe
kuwa unapopiga kura Oktoba 29, unachagua kiongozi unayemwamini atasimama imara
na kuhakikisha bajeti ya miradi kama Bandari ya Bagamoyo haipotei. Kura yako
ndio uhakiki (audit) wa kwanza wa kazi.
Chama Tawala
(CCM) kimetoa ahadi zake. Kura yako ndio tathmini ya utendaji wao.
Wametekeleza? Wapigie kura waendelee! Wamefeli? Wape kura chama kingine! Kura
ndio inayomfanya kiongozi awe mwajibikaji kwako, kijana.
Kwa kupiga
kura unalinda fursa ya ajira yako hasa pale ambapo bahari inakwenda kuwa chanzo
cha fursa kwa kizazi kijacho. Uwekezaji katika meli za uvuvi wa bahari kuu
unahitaji uongozi thabiti. Kura yako inachagua kiongozi anayelinda rasilimali
hizi kwa hekima na kwa manufaa ya muda mrefu, si kwa faida ya muda mfupi.

0 Maoni