MGOMBEA
Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel
Nchimbi, amesema CCM ndiyo chama pekee kilichojidhihirisha kwa Umma,
kinachoweza kuhangaika na matatizo ya wananchi wake.
Dkt.
Nchimbi ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2025 wakati akihitimisha mkutano wake wa
mwisho wa hadhara wa kampeni ,
uliofanyika kwenye uwanja wa Kazegunga katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, ikiwa
ni muendelezo wa kampeni zake zinazoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.
Amesema,
vipo vyama vingi duniani havishughuliki na matatizo ya wananchi wake bali kwa
maslahi yao binafsi na viongozi.
Dkt.Nchimbi
amesema, chama hicho ndicho kimeudhihirishia Umma kuwa ndiyo chama kinachoweza
kuwaletea miradi ya maendeleo wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,
afya, biashara, kilimo na miundombinu ya barabara.
Pia,
ameeleza, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufuata misingi ya CCM ameweza
kuendeleza na kukisimamia chama na kuhakikisha kinaendelea kuwa na misingi
mizuri na chama imara nchini.
Aidha, Dkt.Nchimbi
pia alitumia nafasi hiyo kumuombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo
mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Ndugu Peter Selukamba
pamoja na Madiwani.


0 Maoni