Kamishina
wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos
Silayo, ameongoza kikao na timu ya STEP-Programme ikiongozwa na Mkurugenzi
wa Mkakati wa Usimamizi wa Ikolojia ya Udzungwa, Dk. Trevor Jones, akiambatana
na Meneja wa Ikolojia Frank Linhwa.
Katika
kikao hicho kilichofanyika jana, pande zote zimekubaliana kuanza utekelezaji wa mpango mkubwa wa
uwezeshaji katika ulinzi shirikishi wa misitu, ikiwa ni pamoja na upatikanaji
wa vitendea kazi kama magari, mafunzo kwa watumishi na mikakati endelevu ya
kuhifadhi bioanuai katika eneo la Ndwele. Hatua hii inalenga kuimarisha
jitihada za TFS katika kulinda na kutunza ikolojia inayounganisha Misitu ya
Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Udzungwa na Kilombero.
Aidha,
imeelezwa kuwa matukio kadhaa ya kuimarisha ushirikiano kati ya TFS na STEP
yamepangwa kutekelezwa katika siku zijazo, ili kuhakikisha ikolojia hii muhimu
inabaki salama kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.
0 Maoni