Mamlaka
ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imeadhimisha Siku ya Utalii
Duniani kwa kuwapeleka makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo watoto wenye
mahitaji maalum na wanafunzi kutembelea Hifadhi ya Wamimbiki iliyopo katika
Mikoa ya Morogoro na Pwani kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali vya utalii
vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.
Makundi
hayo yamejumuisha, Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Dar Ul Muslimeen
pamoja na Shule za Msingi na Sekondari za Gwata,Maseyu,Kitungwa, Migogodo na
Kivuge zilizopo Mkoani Morogoro.
Sambamba
na hilo, TAWA imeendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa watalii hao ili kujenga
kizazi kinachopenda uhifadhi na utalii kwa ajili ya kuwa na Utalii wenye
mageuzi na maendeleo endelevu.
Siku ya
utalii duniani inaadhimishwa kila tarehe Septemba 27 na kwa mwaka huu imebeba
kauli mbiu isemayo Utalii na Mageuzi Endelevu.



0 Maoni