Wakala ya Barabara za Vijijini na
Mijini (TARURA) inaendelea kishiriki katika mafunzo yenye lengo la kuimarisha usimamizi wa mikataba ya miradi
ili kupunguza gharama na ucheleweshaji wa miradi.
Mafunzo hayo ya siku tano ambayo
yamewaleta pamoja wadau muhimu katika Sekta ya Ujenzi wa Miundombinu ya
barabara na usafirishaji pamoja na mambo mengine yanalenga kubadilishana uzoefu katika sekta hiyo muhimu
kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Mkurugenzi wa Barabara kutoka
TARURA, Mhandisi Venant Komba amewasilisha mada ya namna TARURA inavyo tekeleza
majukumu yake, mikakati inayotumika katika usimamizi wa miradi, teknolojia
zinazotumika katika ujenzi wa Barabara na changamoto zilizopo katika utekelezaji
wa miradi hasa kipengele cha mikataba ikiwa ni sehemu ya kutoa uzoefu wa Wakala
huo katika eneo hilo muhimu.
Akizungumza wakati wa
uwasilishaji Mhandisi Komba amesema moja kati ya vipaumbele walivyonavyo kama
taasisi ni kujengea wataalamu wao uwezo (capacity building) hasa katika maswala
ya usimamizi wa mikataba ili kuepusha changamoto wakati wa utekelezaji wa
miradi.
“Tunatumia nafasi kama hizi kama
fursa ya kuendelea kujifunza kutoka kwa wenzetu' amesema.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama
cha Barabara Tanzania (TARA) kwa kushirikiana Wahandisi washauri kutoka
ndani na nje ya nchi.
0 Maoni