Msajili wa
Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa, pamoja na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Bw.
Abdallah Mhagama.
Mazungumzo
hayo, ambayo pia yalihusisha wataalamu kutoka taasisi hizo tatu, yalifanyika
katika ofisi za LATRA jijini Dodoma, siku ya Jumatano, Septemba 3, 2025, na yalilenga
kuboresha utendaji kazi wa TRC.
Ofisi ya Msajili
wa Hazina inasimamia jumla ya taasisi na kampuni 308 ambazo Serikali ina hisa.
Kati ya
hizo, taasisi 252 zikiwemo TRC na LATRA ni zile ambazo Serikali inamiliki hisa
nyingi, huku 56 zikiwa ni kampuni ambazo Serikali inamiliki hisa chache.
0 Maoni