Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
na mkewe, Brigitte, wanapanga kuwasilisha ushahidi wa picha na wa kisayansi
katika mahakama ya Marekani ili kuthibitisha kwamba Bi. Macron ni mwanamke.
Wakili wao amesema kuwa rais wa
Ufaransa na Bi. Macron watawasilisha nyaraka hizo katika kesi ya kashfa
waliyoifungua dhidi ya mshawishi wa mrengo wa kulia, Candace Owens, baada ya
Owens kueneza imani yake kwamba Brigitte Macron alizaliwa mwanaume.
Mawakili wa Bi. Owens wamejibu
kwa kuwasilisha ombi la kufuta madai hayo.
Akizungumza na podikasti ya BBC
Fame Under Fire, wakili wa familia ya Macron, Tom Clare, alisema kuwa Bi.
Macron alipata madai hayo kuwa "ya kuhuzunisha sana" na kwamba ni
"usumbufu" kwa rais wa Ufaransa.
Bi. Owens, ambaye ni mchambuzi wa
zamani wa shirika la kihafidhina la Marekani Daily Wire na ana mamilioni ya
wafuasi kwenye mitandao ya kijamii, ameendelea kueneza mtazamo wake kwamba
Brigitte Macron ni mwanaume.
0 Maoni