Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto
Mashaka Biteko amesema kuwa Chama Cha
Mapinduzi kimepata Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais, anayefaa na kujua
majukumu yake ambaye ni Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 6, 2025 wakati akiwasalimia wananchi wa Katoro kwenye
Kampeni za Mgombea Mwenza wa nafasi ya hiyo ya Urais kupitia CCM, Balozi. Dkt.
Nchimbi.
“ Tumepata Mgombea Mwenza anayejua kazi, anayejua shida za
watu yeye ni mwalimu wa wengi nikiwemo mimi ametufundisha mengi,” amesema Dkt.
Biteko.
Ameendelea kubainisha sifa za Dkt. Nchimbi na kusema kuwa ni
mtu mwema anayejua kumuweka karibu kila mtu na ambaye hazungumzii wapinzani
katika hotuba yake ispokuwa CCM, kazi yake na kubadilisha maisha wa wananchi.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo, Dkt. Biteko
amewaeleza wananchi wa Katoro na Geita kuwa Uchaguzi na kura yao ni maisha yao
hivyo amewaomba Oktoba 29 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kupiga kura.
Amesisitiza “ Najua Katoro hamna mbambamba, kwenu nyie hamna
mechi ndogo hata mazoezi kwenu nyie mechi, nawaomba mtuchagulie madiwani na
mbunge ili waungane na Dkt. Samia Suluhu Hassan ili tuweze kuleta maendeleo ya
Katoro na Katoro lazima ibadilike.”
Aidha, amesema Geita inawaunga mkono Dkt. Samia na Nchimbi,
wabunge na madiwani wa CCM na inahusisha Uchaguzi na maisha yao hivyo wanachagua kwa ajili ya
maisha yao.




0 Maoni