Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameungana na mamia ya
waombolezaji kutoa pole kwa familia ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufuatia kifo cha kaka yake Abass
Mwinyi ambaye pia alikuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Fuoni kilichotokea
Zanzibar, Unguja usiku wa kuamkia
Septemba 25, 2025.
Dkt.
Biteko ameshiriki mazishi hayo Septemba 26, 2025 Bumbubwini Mangapwani,
Zanzibar.
Ambapo
ameungana na viongozi mbalimbali akiwemo Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Makamu Mwenyekiti wa CCM
Taifa, Ndugu Stephen Wasira, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Aidha,
baada ya mazishi baadhi viongozi walipata fursa ya kutoa heshima katika kaburi
la Hayati Ali Hassan mwinyi lililopo Bumbubwini Mangapwani, Zanzibar.
Awali,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alifika
msibani kuwafariji wafiwa na kisha kusaini kitabu cha maombolezo.
Na. Ofisi
ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati




0 Maoni