MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amewasili katika uwanja wa Kashai,Bukoba mjini kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni leo Septemba 7, 2025 mkoani Kagera.
Awali leo Dk. Nchimbi ameanza ziara yake ya kampeni Mkoani
humo akianzia Jimbo la Ngara, Kyerwa, Katoro-Bukoba Vijijini na kuhitimisha kwa
mkutano mkubwa jioni hii hapa Bukoba Mjini.
Dk. Nchimbi anaendele na mikutano yake ya kampeni ya kusaka kula za ushindi wa
kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima,ambapo kwa sasa yuko mikoa ya
Kanda ya Ziwa ambapo alianzia mkoani Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita na
sasa yupo mkoani Kagera.
Dk. Nchimbi anaendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
0 Maoni