Maneno hayo yamesemwa jana na Mgombea Mbunge jimbo la
Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akinadi sera na ilani ya uchaguzi ya
CCM mbele ya wanachalinze waliojitokea kwa wingi kwenye mkutano wa ufunguzi wa
kampeni za uchaguzi wa Mbunge huyo katika mji wa Mdaula, Bwilingu.
Akiongea mbele ya wananchi hao Ndg. Kikwete ametumia nafasi
ya jukwaa hilo kuwakumbusha wana chalinze ahadi za ilani ya CCM mwaka 2020 na
jinsi ambavyo wamefanikiwa kutekeleza. Mgombea huyo amewakumbusha mambo sita
ambayo yalikuwa ni kitendawili kwa wananchi hao ikiwemo shida kubwa ya maji,
uchumi na makusanyo, afya, elimu na maendeleo ya jamii. Mgombea huyo wa Ubunge
aliwaelexa wanachalinze mafanikio yaliyokwisha patikana huku akishukuru
ushirikiano mkubwa na uongozi wa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha
utekelezaji wa ilani hiyo kwa hali ya juu.
Kwa upande wa elimu , mgombea aliwakumbusha idadi ya shule
mpya za msingi na sekondari, nyumba za walimu, ukarabati wa shule chakavu
zilizojengwa na kufanyiwa ukarabati. Aliwakumbusha pia kwenye miradi ya afya
hasa programu mbalimbali zilizofanyika jimboni ikiwemo pia ujenzi wa hospitali
ya wilaya, Vituo vya Afya 6, zahanati 54 zilizokwisha jengwa, na kwa upande wa
maendeleo ya jamii masoko, vituo vya afya, mikopo nk.
Mgombea kikwete alitumia jukwaa hili pia kuwakumbusha kuwa
ilani ya CCM imeelekeza mambo mengi mazuri kufanyika ikiwa ni pamoja na
kumalizia kazi ya kupeleka maji kwenye makazi ya wanachalinze, ujenzi wa
mabweni na shule mpya , kilimo kitapewa kipaumbele, mifugo bora, chalinze ya
viwanda, na mengineyo mengi.
Akizungumza kabla hajamkaribisha mgombea kuzungumza mgeni rasmi wa uzinduzi huo Bi. Zainab Vullu amewashukuru wanachalinze kwa ushirikiano mkubwa wanaompa mbunge wao na ndiyo maana mafanikio yanaonekana. Ametumia pia nafasi hiyo kuwaombea kura madiwani wa halmashauri hiyo na Mgombea urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Dr. Samia Suluhu Hassan wa Chama Cha Mapinduzi.
0 Maoni