WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelipongeza Soko la Hisa la Dar
es Salaam (DSE) kwa kuongezeka kwa thamani ya soko hilo na kufikia shilingi
trilioni 21.0 katika kipindi cha kufikia julai 2025.
Amesema kuwa pia soko hilo limeongeza ukuaji wa mauzo ya
hisa kwa zaidi ya asilimia 246 pamoja na ongezeko la idadi ya wawekezaji hadi
zaidi ya akaunti 683,000 ikiwa ni ishara ya ukuaji imara wa sekta ya mitaji
nchini
Amesema hayo leo Jumanne (Agosti 26, 2025) alipotembelea Ofisi za soko hilo zilizopo Morocco, jijini Dar es Salaam.
0 Maoni