Vikundi vilivyopo kata za Pangani ya zamani, Mwera, Pangani
Magharibi pamoja na kata zingine wameshukuru Wakala ya Barabara za Vijijini na
Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE kwa mafunzo waliyopatiwa na fursa za
kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali.
Mafunzo haya yamehusisha ufafanuzi wa kazi ndogo ndogo za
matengenezo ya barabara, elimu ya ujasiriamali, elimu ya namna ya kujisajili na
kutumia mfumo wa manunuzi NEST pamoja na elimu kwa vitendo ya matengezo ya
barabara.
Akizungumza kwa niaba ya wanavikundi wengine, Bw. Kibwana
Athuman amesema “Tunashukuru sana TARURA kwa mafunzo haya yamekuwa na manufaa
kwetu sisi kama vikundi. Tumeona fursa nyingi katika kujihusisha kwenye
matengenezo ya barabara.”
Villevile, Bi Salama Shabani wa kikundi cha Combine ground
ameelezea namna mafunzo haya yalivowasaidia kama wanawake “kweli tunashukuru
kwa mafunzo haya yametufungua macho sisi wanawake kwenye mambo mengi hasa
kutumia mifumo mipya kama NEST”.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa vikundi 38 kwa ushirikiano na
Shikirika la Kazi Duniani (ILO) pamoja na Mamlaka wa Udhibiti wa Ununuzi wa
Umma (PPRA).
Mtaalamu kutoka PPRA, Bw. Magnus Steve ametoa elimu ya namna vikundi hivyo vinavyoweza kujisajili na kutumia mfumo wa manunuzi wa NEST kama fursa ya kupata zabuni mbalimbali katika maeneo ya ndani na nje ya makazi yao.
0 Maoni