Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia
mradi wa Uboreshaji Barabara za Vijijini kwa Ushirikishaji wa Jamii na
Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE) umeendelea kuleta fursa kwa
kuwapatia mafunzo vikundi 14 vya wakazi wa kata ya Pangani ya zamani, wilayani Pangani
mkoani Tanga.
Mafunzo hayo yanalenga kuwapatia vikundi hivyo fursa na
elimu ya umuhimu wa wananchi kushiriki moja kwa moja kwenye matengenezo na
maboresho ya kazi mbalimbali kupitia programu ya CBRM (Community Based Road
Maintenance).
Kupitia programu hiyo wananchi walio wanachama wa vikundi
hivyo watapata fursa ya kukua kichumi na kijamii kupitia mafunzo mbalimbali na
ajira kwa vikundi hivyo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa TARURA wilaya
ya Pangani, Mhandisi Mwita Muhochi ameeleza umuhimu wa ushirikishwaji wa
wananchi katika matengenezo na utunzaji wa miundombinu ya barabara.
Aidha, Mhandisi Delchance Nuru kutoka Timu ya mradi wa RISE,
ameeleza kuhusu mradi wa RISE na kufafanua zaidi kuhusu programu kwa vikundi
hivyo.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa kuhusisha mafunzo ya darasani pamoja na kujifunza kwa vitendo.
0 Maoni