Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa
Ndugu Ismail Ali Ussi amewapongeza wafanyakazi wa TARURA wilaya ya Musoma kwa
kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanajenga miradi ya miundombinu ya
barabara kulingana na thamani halisi ya fedha.
Ndugu Ussi ameyasema hayo wakati
akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya Nyabisarye Mahakama kuu
Kanda ya Musoma yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami.
Ussi amesema kuwa
Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu
ya barabara kwa lengo la kuwarahisishia wananchi huduma katika maeneno yao ili
waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi na kujiingizia kipato.
Kwa upande wake Kaimu
Meneja Wilaya ya Musoma Mhandisi Mohamed Etanga amesema jumla ya shilingi
Milioni 600.97 zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya
Nyabisarye- Mahakama Kuu yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami.
Amebainisha kuwa ujenzi wa barabara
hiyo ulianza Oktoba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba,
2025.
Mhandisi Etanga ameongeza kusema kuwa
barabara hiyo endapo itakamilika itakuwa kiunganishi cha Kata ya Bweri na Kata
ya Rwamlimi na kuwa kiungo kikubwa kwa wananchi katika kupata mahitaji ya
kijamii kwa wepesi.
0 Maoni