Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba
wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United
Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid. Mgombea huyo waaliambatana na
Mgombea Mwenza, Mhe. Juma Khamis Faki (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti
15, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kulia ni
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. (Picha na INEC).
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party
(UDP), Mhe. Swaum Hussein Rashid akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Juma Khamis Faki
(kushoto) wakionesha beki la fomu za uteuzi walililokabidhiwa na Tume.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party
(UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akielekezwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC,
Ndg Ramadhani Kailima namna ya kusaini kitabu.
0 Maoni