Rais Trump acharuka wimbi la uhalifu Washington DC

 

Rais Donald Trump amesema atapeleka mamia ya wanajeshi wa Kikosi cha Uliniz wa Taifa (National Guard) huko Washington DC na kuchukua udhibiti wa idara ya polisi ya jiji hilo ili kukabiliana na wimbi la uhalifu. 

Katika mkutano na waandishi wa habari, alitangaza "Siku ya Ukombozi" kwa jiji hilo na akaahidi "kuokoa mji mkuu wa taifa letu kutokana na uhalifu, umwagaji damu, machafuko, uchafu na hali mbaya zaidi". 

Hata hivyo, Meya wa Washington DC, Muriel Bowser, amesema kuwa jiji hilo "limeshuhudia kupungua kwa kiasi kikubwa kwa uhalifu" na kwamba "liko katika kiwango cha chini cha uhalifu wa kutumia nguvu katika kipindi cha miaka 30".

Chapisha Maoni

0 Maoni