Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imehitimisha maadhimisho ya siku ya askari Wanyamapori duniani kwa kufanya michezo mbalimbali iliyohususu askari wa Jeshi la Uhifadhi, askari wa Jeshi la polisi wilaya ya Karatu pamoja na kufanya shughuli ya upandaji miti katika shule ya Sekondari Welwel iliyopo Karatu Mkoani Arusha.
Kamishna wa Uhifadhi NCAA
ameongoza maafisa na askari katika zoezi la kupanda miti Shule ya Sekondari
Welweli, kutoa elimu ya shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa wanananchi
na kuongoza watumishi hao katika michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia kilomita
tano, mchezo wa mpira wa miguu kati ya askari wa jeshi la Uhifadhi kutoka pori
lla akiba Pololeti, askari walioko eneo la hifadhi ya Ngorongoro pamoja na
Polisi Karatu.
“NCAA ni sehemu ya Jamii,
katika utekelezaji wa majukumu yetu tunashirikiana na vyombo vingine ikiwepo
Polisi Wilaya za Ngorongoro na karatu pamoja na wananchi, ndio maana leo
tumefanya michezo ya riadha, mazoezi yaa viungo, mchezo wa mpira wa miguu ili kuendelea
kutuweka pamoja hasa katika shughuli za kuimarisha usalama na ulinzi wa
rasilimali za Nchi) alifafanua Kamaishna Badru.
Badru ameeleza kuwa NCAA
pia ina jukumu la kutoa elimu ya mazingira na uhifadhi shirikishi kwa jamii
zinazozunguka hifadhi ya Ngorongoro, hivyo katika kuadhimisha siku ya askari wa
Wanyamapori imetoaa miti bure kwa wananchi ili wakapande katika maeneo yao na
kupanda miti katika shule ya Sekondari Welwel kisha kuzungumza na walimu na
wanafunzi wa shule hiyo na kuwasisitiza kutunza miti iliyopandwa pamoja na
mazingira kwa ujumla.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Katibu tawala wa Wilaya hiyo Bw. Bahati Mfungo
ameipongeza NCAA kwa ushirikiano inaotoa kwa wananchi wa Wilaya ya Karatu hasa
kuwapa elimu ya mazingira, upandaji miti, kupambana na mgongano kati ya
Wanyamapori na wananchi pamoja na kusaidia miradi mbalimbali ya wananchi
ikiwemo huduma za kijamii.
Siku ya Askari wa
Wanyamapori Duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuwakumbuka
askari waliopoteza maisha wakati wa kutekeleza majukumu yao, kauli mbiu ya
maashimisho ya mwaka huu ni “ Rangers: Powering Transformative
Conservation” ikilenga kuutambua mchango
wa askari wa Wanyamapori katika kuleta mabadiliko ya kweli katika uhifadhi wa
maliasili ambayo ni urithi wa Taifa.
Na. Philomena Mbirika -
Karatu Arusha
0 Maoni