Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Viongozi Wanawake
Duniani (WPL) na aliyekuwa Mbunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Neema Lugangira, Agosti 23,2025 amekutana, kuzungumza na
kusalimiana na kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV, kwenye Makazi yake Jijini Vatican nchini
Italia.
Lugangira amekutana na Papa Leo XIV siku chache baada ya
kuteuliwa rasmi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya WPL yenye makao yake makuu
Jijini Brussels nchini Ubelgiji akiwa Mtanzania wa kwanza kuhudumu kwenye
Jumuiya hiyo ya Kimataifa.
Lugangira ni miongoni mwa viongozi kutoka Tanzania wanaoongoza taasisi kubwa za kimataifa duniani, pamoja na mambo mengine kiongozi huyo anatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kiuongozi.
0 Maoni