Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, kupitia
taarifa iliyotolewa hivi punde na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi,
Amos Makalla, imetangaza mabadiliko muhimu ya uongozi ndani ya chama.
Katika mabadiliko hayo, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
imemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Katibu Mkuu wa CCM, nafasi ambayo ilikuwa
ikishikiliwa na Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa
urais.
Aidha, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi, kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo. Uteuzi huu unamuweka Kihongosi kuchukua nafasi ya Amos Makalla, ambaye alikuwa akishikilia wadhifa huo hadi sasa.
0 Maoni