Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekusanya
zaidi ya Sh86 bilioni katika harambee ya kukichangisha fedha kwa ajili kampeni
za Uchaguzi Mkuu wa utakaofanyika Oktoba 2025 pamoja na ujenzi wa chama hicho.
Harambee hiyo imefanyika jana usiku
Agosti 12, 2025 katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambapo
mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia Rais Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo
zilizochangishwa katika harambee hiyo Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi
amesema kati ya kiasi hicho Sh 56.3 bilioni ni fedha taslimu na Sh 30 bilioni
ni ahadi. Malengo ya harambee hiyo ilikuwa ni kukusanya Sh100 bilioni.
Akiongea katika harambee hiyo Rais
Dkt. Samia amewapongeza wote waliotoa fedha na kusema zitasaidia katika kampeni
za uchaguzi zitakazoanzia Agosti 28 hadi Oktoba 28, 2025, ambapo siku Jumatano
ya Oktoba 29, 2025 wananchi watapiga kura.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongea jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wakatika wa Harambee ya CCM iliyofanyika jana usiku Agosti 12, 2025 katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
0 Maoni