Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi leo Agosti 31, 2025 amewahutubia
Wananchi wa Rorya waliofurika katika uwanja wa Ubwere, ikiwa ni muendelezo wa
mikutano yake ya Kampeni kwenye mikoa ya kanda ya ziwa.
Balozi Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Rorya, Jafari Chege
sambamba na Wagombea Ubunge wengine pamoja na Madiwani wa Mkoa huo.
Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.
0 Maoni