Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukombe, Zedekiah Solomon
Osan amemkabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bukombe
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Agosti 26, 2025
katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bukombe - Mkoani Geita.
Makabidhiano hayo ya fomu ni utekelezaji wa ratiba kuelekea
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka 2025 Aidha, Maelefu ya wana CCM na
wapenzi wa chama hicho wamemsindikiza mgombea kwa ajili ya kuchukua fomu kwa
ajili ya kuomba kuteuliwa na Tume huru ya Uchaguzi.
Katika hali isiyo ya kawaida, zaidi ya wanama 1000
wamejotokeza kumdhamini Dkt. Biteko ikilinganishwa na mahitaji ya wadhamini 31
waliohitajika kisheria.
Akizungumza na wanaCCM katika viwanja Ofisi ya CCM Wilaya ya
Bukombe, Dkt. Biteko amewataka wananchi kudumisha mshikamano na upendo miongoni
mwao na kuwachagua viobgozi bora.
“ Utakapofika wakati tuwaxhague viongozi tunaowapenda,
nawaomba mmchague Dkt. Samia Suluhu
Hassan kuwa Rais, Mnichague mimi kuwa mbunge na niwaaombe mbiletee madiwani wa
CCM kwa tuendeleze kazi tuliyokwisha ianza.”
Awali, Katibu wa CCM, Wilaya Bukombe Leonard Mwakalukwa
amesema wana CCM zaidi ya 3500 wamejitokeza kumsindikiza mgombea katika Ofisi
za tume huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu.
Amesema wadhamini 31
kutoka Kata zote 17 za Bukombe wamewawakilisha wenzao 969 waliojitokeza
kumdhamini mgombea.
0 Maoni