Wafanyabiashara Dar wapo tayari kuhudumia wageni wa CHAN

 

Kuelekea michuano ya CHAN 2024 inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo Agosti 02, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Saalaam, Wafanyabiashara  wa Jiji  hilo wamesema wamejiandaa vizuri kuwahudumia  wageni wa mashindano ya CHAN 2024 kwa kuonesha ukarimu wa Watanzania.

Kwa upande watoa huduma ya  chakula wamesema wanafurahia ujio wa mashindano ya CHAN nchini sababu wana uhakika watanufaika katika biashara zao.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya utoaji wa huduma hiyo Julai 29,2025 Mwenge Dar es Salaam, Mpishi wa Mgawa wa  AFCON 2027 Bw. Hussein  Omary alisema, amejipanga vizuri kuandaa vyakula mbalimbali  vya Kitanzania na vya asili ya Afrika.

“Tunawakaribisha wageni wote wa CHAN kwenye mgahawa wetu  ambao tayari tumeanza kuitangaza AFCON 2027,  tumejiandaa vizuri kuwapatia huduma bora ya vyakula vya asili ya Kitanzania na Afrika,"alisema Hussein.

Michuano ya CHAN hapa nchini itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na New Amaan Zanzibar kwa kiingilio cha shilingi  VIP A - 10,000, VIP B & C 5000   na mzunguko 2000.



Chapisha Maoni

0 Maoni