Kamati Kuu ya Halmashauri
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imempitisha Mfanyabiasha maarufu Salum Moud Kinyoro
'Kibakuli' kuwania ubunge wa Jimbo la Handeni Mjini pamoja na wagombe wengine
watano.
Wagombe wengine
waliopitishwa katika jimbo hilo ni Kwagilwa Reuben, Mariam Gerald, Sonia Juma,
Hafidhi Seif pamoja na Hamis Hamad.
Katibu wa Itikadi na
Uenezi, Amos Makala ametangaza majina hayo
leo Julai 29, 2025.
0 Maoni