Mji wa Songea unasimama
kama ngome ya kihistoria, ukihifadhi kumbukumbu ya mashujaa waliomwaga damu yao
kupigania uhuru wa Tanganyika kupitia Vita ya Majimaji (1905–1907) — vita ya
kwanza kubwa ya kisasa ya waafrika dhidi ya ukoloni barani Afrika!
Mashujaa 67 walinyongwa
kwa kosa moja: KUPINGA UKOLONI!
Mashujaa 66 walizikwa
kwenye kaburi moja—ishara ya mshikamano wa kweli. Na shujaa mkuu, Nduna Songea
Mbano, alizikwa peke yake kwa heshima kubwa. Leo, kaburi lake linaheshimiwa
ndani ya Makumbusho ya Majimaji, makumbusho pekee nchini Tanzania yanayohifadhi
urithi halisi wa vita vya ukombozi.
Jina la Songea linabeba
urithi wa Nduna Songea Mbano, shujaa wa kweli. Kupitia historia hii ya kipekee,
Songea inajitokeza kama kituo muhimu cha utalii wa kihistoria na kiutamaduni.
0 Maoni