Mh. Mavunde awasili Namtumbo kwenye Mgodi wa Urani

 

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amewasili Wilaya ya Namtumbo,Mkoani Ruvuma leo kwa ajili ya ukaguzi wa maandalizi ya ziara ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mradi wa madini ya Urani unaotekelezwa na Kampuni ya Mantra Tanzania Ltd.

Tarehe 30.07.2025 Mh. Rais Dkt. Samia atazindua Kiwanda cha Uchenjuaji madini ya Urani na pia atazindua rasmi kuanza kwa ujenzi wa mgodi wa Urani na ujenzi wa Mtambo mkubwa wa kuchenjua madini ya Urani ambao unakadiriwa kuwa gharama ya zaidi ya Tsh 3.06 Trilioni.




Chapisha Maoni

0 Maoni