Dkt. Biteko hana mpinzani ubunge ndani ya CCM

 

Kamati Kuu ya Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, imepitisha jina la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko kuwa mgombea pekee wa ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya chama hicho.

Dkt. Biteko ni miongoni wa wagombea wachache waliobahatika kupita bila ya kupata mpinzani ndani ya CCM, ambapo wengine waliopata bahati hiyo ni pamoja na Mama Salma Rashid Kikwete Jimbo la Mchinga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Jakaya Kikwete Jimbo la Chalinze na Hamad Chande Jimbo la Kojani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, ametangaza leo Julai 29, 2025 majina yote ya wagombea waliopitishwa baada ya kuomba kupendekezwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

Chapisha Maoni

0 Maoni