WAZIRI MKUU, Mhe. Kassim
Majaliwa ametembelea kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Sanganigwa
kilichopo mjini Kigoma, kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Kigoma.
Akizungumza na watoto
na walezi wa kituo hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali
inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa madhehebu ya
dini katika kuwalea kimwili na kiroho watoto wenye mahitaji maalum nchini.
“Kwa niaba ya Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan, ninalishukuru kanisa katoliki jimbo la Kigoma, mtu
mmoja mmoja na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa Serikali
katika kuwalea watoto wetu, hakika mnafanya jambo kubwa na lakumpenda Mungu na
wanadamu.”
Akisoma taarifa ya
kituo hicho kwa Waziri Mkuu jana Juni 13, 2025, Mkurugenzi wa Kituo hicho
Keneth Hageze amesema kuwa kilianzishwa mwaka 1995 na mpaka sasa kimehudumia
watoto 1309.
Mheshimiwa Majaliwa
alitoa Mchele, Maharage, Mafuta, Sukari pamoja na Taulo za kike.
0 Maoni