Wakala ya Barabara za
Vijijini na Mijini (TARURA) inashiriki kwenye maonesho ya madini na fursa za
uwekezaji yanayofanyika katika uwanja wa madini wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Akizungumza katika
mahojiano maalum, Meneja wa TARURA mkoa wa Lindi, Mhandisi Fanuel Kalugendo
ameeleza kuwa TARURA inaendelea kutekeleza ujenzi wa barabara zitakazofungua
migodi inayopatikana katika wilaya hiyo ambapo barabara hizo zitajengwa kupitia
mradi wa RISE unaogharamiwa na mkopo nafuu toka Benki ya Dunia.
Barabara hizo
zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni barabara ya Ruangwa - Mbwemkuru (Km 31)
na barabara ya Nandagala - Mpiruka - Nachingwea (Km28) zilizopo wilayani
Ruangwa.
Ameeleza kuwa
wananchi mbalimbali wameendelea kufika katika banda la TARURA na kujionea kazi
nzuri zinazofanywa na wakala katika kuboresha mtandao wa barabara mkoa wa
Lindi.
Maonyesho hayo
yaliyoanza tarehe 11 Juni, 2025 yamelenga kuonesha na kuwaelimisha wananchi
fursa zilizopo wilaya ya Ruangwa hususani katika sekta ya madini.
Maonyesho hayo
yanatarajiwa kufungwa leo siku ya Jumamosi tarehe 14 Juni, 2025 na Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
0 Maoni