Wanamichezo kutoka
mikoa mbalimbali wamewasili katika viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa
kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2025.
Ufunguzi huo
unatarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Kassim Majaliwa leo Tarehe 9 Juni 2025.
Mashindano ya
UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 yanafanyika kitaifa Mkoani Iringa, ikiwa ni
baada ya kufanyika katika Tabora kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2022 hadi
2024.
UMITASHUMTA &
UMISSETA inaandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utamaduni
na Michezo. 
Kauli mbiu ya
Mashindano ya mwaka huu ni "Viongozi bora ni msingi wa maendeleo na
Taaluma, Sanaa na Michezo,Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa
Amani na Utulivu."
Na. OR-TAMISEMI 

 
 
 
 
 
 
 
 
0 Maoni