TRC kuanza kusafirisha mizigo kwa SGR kesho

 

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuwa linaanza rasmi huduma ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli ya kisasa ya SGR kuanzia kesho Juni 27, 2025.

Taarifa ya TRC iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Fredy Mwanjala imesema huduma hiyo itafanyika kati ya Stesheni ya Pugu Dar es Salaam na Stesheni ya Ihumwa ya Dodoma.



Chapisha Maoni

0 Maoni