Wakala ya Barabara za
Vijijini na Mijini (TARURA) imetunukiwa tuzo maalum ya ushirikishaji jamii
katika ujenzi wa barabara yaani " People Centered Design Approach".
Ushirikishaji huo ni
kuhakikisha usanifu unajumuisha mawazo, mapendekezo na mahitaji maalum kwaajili
ya jamii itakayohudumiwa na barabara husika baada ya kujengwa hususani maeneo
ya shughuli za kijamii kama shule, masoko na huduma za afya (hospitali, vituo
vya afya, zahanati na kliniki).
Tuzo hiyo maalum
imetolewa na Taasisi ya Kimataifa ya ‘FIA Foundation' kwa kushirikiana na AMEND
katika kongamano la Kikanda la Afrika lililofanyika katika hoteli ya Hyatt
Regency jijini Dar es Salaam lililohudhuriwa na nchi mbalimbali ikiwemo Ghana,
Ivory Coast, Kenya, Zambia, Msumbiji, Afrika ya Kusini, Sao Tome, Madagascar na
mwenyeji Tanzania.
TARURA imeshiriki
kongamano hilo kwa kutoa elimu kwa nchi mbalimbali za kiafrika ili kuhakikisha barabara
zinazojengwa zinakuwa salama kwa watumiaji hususani watoto wa shule.


0 Maoni