Serikali ya Tanzania
imeanza mashauriano na maafisa wa Marekani kujua maeneo yanayotakiwa kufanyiwa
maboresho ili kuhakikisha Tanzania isiwe moja ya nchi ambazo raia wake watazuiliwa
kuingia Marekani.
Taarifa iliyotolewa
leo na Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji
Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa imesema mashauriano hayo yanalenga kujua maeneo
ambayo yanatakiwa kufanyiwa maboresho hususan yanayohusiana na masuala ya
kikonseli.
Mashauriano haya
yanakuja wakati ambapo Marekani imekuwa ikichunguza na kuweka vikwazo vya visa
kwa baadhi ya nchi kutokana na masuala ya usalama na utawala bora.


0 Maoni