Sekreterieti ya
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ikiongozwa na Mwenyekiti
wake, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi,
imekutana katika kikao chake maalum leo Jumamosi tarehe 28 Juni 2025, kufuatilia
mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi ndani ya CCM.
Kikao hicho kilipokea
na kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za zoezi hilo la uchukuaji wa fomu
za kuwania uteuzi wa kugombea nafasi za uwakilishi katika vyombo vya dola,
lililoanza rasmi leo kwa mchakato wa ndani ya CCM, katika maeneo yote nchi nzima.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa awali, ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu hizo za kuwania
kuteuliwa ndani ya CCM, imeanza leo tarehe 28 Juni 2025, saa 2:00 asubuhi na
itahitimishwa tarehe 2 Julai 2025, saa 10:00 jioni.
Ratiba hiyo
itahusisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi nafasi za; Ubunge
wa Jimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ubunge wa Viti Maalum, Ujumbe wa
Baraza la Wawakilishi Viti Maalum, Udiwani wa Kata au Wadi na Udiwani wa
Viti Maalum.




0 Maoni