Nyota wa Kimataifa
(mstaafu) wa mchezo wa soka Zlatan Ibrahimović, aliestaafu soka katika klabu ya
AC Milan ya Italia ametembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti jana tarehe 11 Juni
2025.
Kutokana picha
aliyoichapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram (@iamzlatanibrahimovic),
Ibrahimović ameonekana amekaa kwenye msingi wa jiwe hilo mkono wa kushoto kuna
maandishi yaliyocharazwa “Serengeti Shall Never Die”, akifurahia mandhari ya
kuvutia ya hifadhi hiyo maarufu duniani.
Ujio wa Ibrahimović
nchini Tanzania ni ishara ya mvuto mkubwa wa Hifadhi za Taifa Tanzania Duniani,
hususan Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa wageni mashuhuri, na umaarifu huo unatoa
fursa ya kuitangaza sekta ya utalii ndani
na nje ya Tanzania kupitia ushawishi wa watu maarufu duniani (Influencers).
0 Maoni