Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI na aliyekuwa Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Juni 30, amejitokeza kuomba ridhaa kwa Chama chake- Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchaguliwa kuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.
Mhe. Mchengerwa
amefika kwenye ofisi ya Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rufiji katika Mji
wa Utete kilomita takribani 60 kutoka barabara kuu ya Dar es Salaam - Lindi
kuchukua na kisha kukabidhiwa fomu ya
kuomba ridhaa kutoka kwa Katibu wa CCM
Wilaya ya Rufiji na baada ya kukamilisha taratibu zote akairejesha.
Mhe. Mchengerwa
aliambatana na mama yake mzazi, ambapo baada ya kuwasilisha fomu asema ameamua
kutumia haki ya kuchagua na kuchaguliwa
ili aendelee kuwaletea maendeleo wananchi wa Rufiji na kisha akaondoka.
0 Maoni