Mapadri 11 kutoka
parokia mbalimbali za jimbo katoliki Singida leo tarehe 18 Juni, 2025 wamefanya
ziara ya kutembelea vivutio vya vya utalii katika hifadhi ya Ngorongoro na
kusisitiza uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kuendelea kuvutia wageni
wengi.
Kiongozi wa mapadri
hao Padri John Makabe ameeleza kuwa, ziara yao imelenga kuona maajabu wa Mungu
aliyoyaumba katika hifadhi ya Ngorongoro, vivutio vya utalii kama wanyamapori,
malikale na mandhari mbalimbali zilizopo
ili kwa nafasi zao wahamasishe jamii umuhimu wa uhifadhi na kutunza mazingira kwa manufaa ya wanadamu
wote.
“Tumekuja kuona
mazingira na kuhimiza utunzaji wake, neno la Mungu katika kitabu cha mwanzo
tumeambiwa Mungu aliumba vitu vyote na kuwakabidhi binadamu ili wavitunze na
kuvilinda, sisi watumishi wa mungu ni
sehemu ya utume wetu kuelezea habari ya umuhimu wa kutunza mazingira,
ziara yetu hapa Ngorongoro imetusaidia
kuona ukweli wa maajabu ya Mungu kupitia hifadhi hii, tutaendelea
kuhamasisha watu kutambua umuhimu wa mazingira kama zawadi tuliyopewa na mungu
ili tuyatunze na yenyewe yatutunze kwa vizazi na vizazi” amesema Padri Makabe.
Akipokea ujumbe wa
mapadri hao, Kamishna Msaidizi mwandamizi anayesimamia huduma za Utalii na
Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kupokea
wageni wengi wa ndani na nje ya nchi na kubainisha kuwa jitihada za Serikali na
wadau wa sekta binafsi kutangaza vivutio vya utalii nchini zimeendelea kuzaa
matunda ambapo uongozi wa NCAA unahakikisha kuwa wageni wote wanapata huduma
bora na kufurahia shughuli za utalii wanapokuwa ndani ya hifadhi.
Na. Kassim Nyaki -
NCAA
0 Maoni