WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 29, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano la Afrika Mashariki la Amani lililoandaliwa na The Islamic Foundation pamoja na Safina Islamic Foundation, katika viwanja vya shule ya msingi Mirongo jijini Mwanza.
Kongamano hilo ni
jukwaa muhimu la kuwaleta pamoja viongozi wa dini, wataalamu, vijana, wanawake
na wadau wa maendeleo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki ili
kujadili masuala ya msingi yanayogusa jamii kwa ujumla.
0 Maoni