Aliyekuwa Diwani wa Kata wa Makurumla Bakari Kimwanga, amechukua na kurudisha fomu kutetea udiwani Makurumla kwa kipindi kingine cha miaka mitano iwapo atapatiwa ridhaa tena na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kimwanga ambaye
ameiongoza Kata hiyo ya Makurumla kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha
miaka mitano iliyomalizika amekabidhi fomu yake hiyo leo Juni 29, 2025 kwa
Katibu wa Kata wa CCM Makurumla, Omari Suleiman Bakari.
Akizungumza baada ya
kukabidhi fomu hiyo, Kimwanga ambaye pia ni mwanahabari alisema kuwa anajivunia
kazi kubwa aliyoifanya kwa miaka mitano na sasa anaomba fursa kwenye
kukamilisha maeneo yaliyobaki ili kujenga jamii yenye ustawi.
"Ninamaliza
miaka mitano ya mafanikio ambapo sisi Makurumla tumefanikiwa kutekeleza miradi
ya zaidi ya shilingi bilioni 18 ikiwamo ya barabara, kituo cha afya na elimu,”
alisema Kimwanga na kuongeza,
"Miaka mitano
ijayo tunakwenda kujenga kata yenye kasi zaidi na muonekano mkubwa wa maendeleo
kwa jamii, wana Makurumla na wana CCM ni watu wema sana nyakati zote tumekuwa
pamoja na Mungu akipenda ikiwa chama itawapendeza jina likarudi kwenye uteuzi
sina shaka na maamuzi yao kwangu na chama chetu ni ushindi."
0 Maoni