Naibu Waziri Mkuu na
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Doto Biteko Juni 29, 2025 amewasili Kigali nchini
Rwanda kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano unaohusu masuala ya nyuklia
Afrika.
Katika Mkutano huo
unaotarajiwa kuanza Juni 30 hadi Julai 1, 2025
nchini humo unajumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika
wenye lengo la kuharakisha matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya
kisasa ili kuleta mabadiliko ya nishati Afrika.
Pamoja na ushiriki
wake katika Mkutano huo Dkt. Biteko anatarajiwa kufungua mjadala wenye mada
kuhusu nishati Afrika na utashi wa kisiasa.
Aidha, katika Mkutano
huo Dkt. Biteko ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi wa Tume ya Mionzi ya Atomiki,
Prof. Najat Mohamed.
Na. Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
0 Maoni