Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF), linampongeza Dk. Kaanaeli Kaale kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti
wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA).
Taarifa iliyotolewa
leo na Mwenyekiti wa TEF Bw. Deodatus Balile imesema uchaguzi huu ni ushuhuda
wa imani kubwa waliyonayo wanahabari wanawake kwake kutokana na mchango wake
thabiti katika tasnia ya habari.
“TEF inaamini kuwa
chini ya uongozi wa Dk. Kaale, TAMWA itaendelea kuwa sauti imara ya kupigania usawa
wa kijinsia, haki za wanawake na ustawi wa wanahabari nchini. TEF inaahidi
kuendeleza ushirikiano kwa TAMWA, huku ikimtakia kila la heri Dk. Kaale katika majukumu
yake mapya,” amesema Bw. Balile.
Pia, Jukwaa la
Wahariri Tanzania limempongeza Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Joyce Shebe
kwa kuifikisha TAMWA kwenye mafanikio makubwa.
Mungu aendelee
kuijaalia kila la heri tasnia ya habari nchini, imemalizia taarifa hiyo.
0 Maoni